Fikiria unatumia masaa kibao kutengeneza post za Instagram, Twitter au TikTok, lakini unapata views, likes, shares, comments kidogooo, followers ndio kabisaaa hupati. Najua hisia hii vizuri sana kwa sababu nimepitia hapo.
Jina langu ni Gillsant Mlaseko, Mtaalam wa masoko mtandaoni kwa miaka 17. Miaka iliyopita, juhudi zangu za kuwasaidia wateja wangu kwenye mitandao ya kijamii hazikuwa zikileta matokeo.
Nilikuwa na hasira. Nilijaribu kila kitu – kama kupost mara kumi kwa siku, kuomba watu wa like na kukomet, ku dance kwenye videos, kulipia matangazo, hadi kununua followers – lakini hakuna kilichofanya kazi.
Nilikuwa nikipoteza muda wangu na pesa kwenye mikakati ambayo haikuleta matokeo ninayohitaji. Nilipoteza kabisa matumaini, lakini sikukata tamaa. Hapo ndipo nilipogundua kuwa nilihitaji mbinu tofauti.
Nilijua kwamba lazima kuwe na njia bora, hivyo nilitumia miezi kutafiti, kupima, na kuboresha mikakati tofauti.
Niligundua kuwa kujenga uwepo mzuri kwenye mitandao ya kijamii siyo tu kupost mara kwa mara – Ila ni lazima utumie mbinu sahihi kwa wakati sahihi.
Baada ya majaribio na makosa mengi, nilitengeneza kile ninachokiita PILAU Formula 2.0 – mfumo wa hatua kwa hatua uliobadilisha mitandao ya kijamii ya wateja wangu kutoka kupoteza muda na kua smaku ya wateja. Hatimaye nilianza kuona matokeo:
Followers walianza kukua kwa kasi. Post zikaanza kufika kwa watu wengi, kupata likes, views, shares, comments za kumwaga. Zaidi ya yote, mauzo yalipanda kwa kasi sana!
Sasa, niko hapa kukushirikisha hii formula iliyothibitishwa na kujaribiwa na wafanyabiashara Pamoja na watu wengine 409 na kuonyesha mafanikio makubwa.